Wanawake wanavyotumia mitandao ya kijamii kuleta ushawishi katika jamii
2024-01-27 09:00:05| CRI

Wiki mbili zilizopita katika kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake, tulizungumzia kuhusu mitandao ya kijamii na jinsi wanawake wanavyopambana katika kutumia mitandao hiyo licha ya changamoto wanazokutana nazo. Ni kweli kwamba wanawake wanakabiliwa na changamoto kubwa hususan katika mitandao ya kijamii, lakini wakati huohuo, hawajakubali kubaki nyuma, kwani wanaitumia mitandao hiyo kuleta ushawishi chanya katika jamii.

Ni kweli, kuna wanawake wanasiasa wanaotumia mitandao ya kijamii kueleza harakati zao, na hivyo kuwapa moyo wanawake na wasichana wengine wanaotaka kuingia kwenye ulingo wa siasa, pia kuna wanawake wanajsiriamali ambao wanatumia mitandao ya kijamii kufahamisha jinsi ya kujipanga katika biashara na pia kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao. Wanawake wamekuwa chachu kubwa katika kuelimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii, hivyo katika kipindi chetu cha Ukumbi wa Wanawake leo hii tutaangazia jinsi wanawake wanavyotumia mitandao ya kijamii kuleta ushawishi chanya kwa jamii.