Wimbo mpya wa Diamond (MAPOZI) haushikiki
2024-01-29 23:31:35| cri

Jamii ya burudani imekunwa na wimbo bora wa Bongo Flavour ulioshirikisha wasanii watatu maarufu Nasseb Abdul (Diamond Plutnumz), Khery Rajab (Mr. Blue) na Sharif Juma (Jay Melody).

Wimbo huo uliopewa jina la ‘Mapoz’ tayari umesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku maelfu ya watu wakipata fursa ya kuisikiliza ili wasibaki nyuma. Hakuna shaka kuwa linapokuja suala la Tasnia ya Bongo Flavour, watatu hao ni moto wa kuotea mbali sokoni kiasi kwamba wana wafuasi wengi wanaowafuata.

Mashabiki wao wengi ndani na nje ya nchi unafanya umaarufu wao uwe mkubwa si ajabu wanapopewa nafasi ya kutaja wasanii watano bora wa Bongo Flavour nchini Tanzania, bila shaka majina yao hayawezi kukosekana kwenye orodha hiyo.

Ukiwa umezinduliwa Alhamisi usiku, wimbo huo ni mpya na jambo zuri kuhusu wimbo huu ni kwamba mashairi ni rahisi kuelewa na kufanya iwe rahisi kwa watu kuuelewa kikamilifu bila wasiwasi.