Tanzania na China zasaini mkataba kwa ajili ya mradi wa eneo la jiolojia la Ngorongoro-Lengai
2024-01-29 10:48:00| cri

Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesaini makubaliano na serikali ya China yakilenga kuendelea na utekelezaji wa mradi wa eneo la jiolojia la Ngorongoro-Lengai.

Taarifa iliyotolewa wikiendi imesema kwamba mradi huo, wenye thamani ya shilingi bilioni 25, umesainiwa na kamishna wa NCAA, Richard Kiiza na kaimu balozi wa China nchini Tanzania Chu Kun.

Mradi huo utajumuisha ujenzi wa miundo mbinu ya utalii huko Miamba na unatarajiwa kukamilika Juni 2025.