ECOWAS yathibitisha Burkina Faso, Mali, Niger kuwa wanachama licha ya madai ya wanajeshi waliopindua serikali
2024-01-29 08:41:13| CRI

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) yenye nchi wanachama 15, imesisitiza kuwa Burkina Faso, Mali, na Niger ni wanachama wa jumuiya hiyo, wakijibu tamko la awali la mamlaka za kijeshi katika nchi hizo, kueleza nia ya kujiondoa uanachama kwenye jumuiya.

ECOWAS imesema katika taarifa yake kuwa haijapokea taarifa yoyote ya moja kwa moja kutoka kwa nchi hizo tatu kuhusu nia yao ya kujitoa kwenye jumuiya hiyo.

Mapema Jumapili viongozi wa kijeshi walitangaza kwenye televisheni za taifa za Mali na Niger, na kuzua wasiwasi miongoni mwa jumuiya ya kimataifa.

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea katika nchi hizo, ili kuhimiza kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba, ECOWAS, imeweka vikwazo vikali kwa nchi hizo tatu tangu jeshi litwae madaraka.