Marais wa China na Ufaransa watumiana salamu za kupongeza miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi
2024-01-29 08:58:29| Cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wametumiana salamu za kupongeza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi zao.

Rais Xi amesema katika miaka 60 iliyopita, China na Ufaransa zimeshikilia chaguo la kimkakati la kujiamulia mambo, na siku zote zinashughulikia kupata maendeleo ya pamoja kupitia ushirikiano wa kunufaishana, kuhimiza mahusiano ya ustaarabu kupitia mawasiliano yenye usawa, na kukabiliana na changamoto za kimataifa kupitia uratibu wa pande nyingi. Amesisitiza kuwa zikiwa ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Ufaransa zinapaswa kuwajibika, na kuanzisha njia ya maendeleo ya binadamu ya kuelekea amani, usalama, ustawi na maendeleo.

Rais Macron amesema kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na China miaka 60 iliyopita ulikuwa ni uamuzi wa kihistoria wenye mtazamo wa mbali, wakati sasa dunia inakabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa, Ufaransa na China, na Umoja wa Ulaya na China zinapaswa kusonga mbele bega kwa bega, ili kutafuta njia ya kukabiliana na changamoto hizo.