Umoja wa Mataifa watoa wito wa ufadhili zaidi kuunga mkono jeshi la Somalia
2024-01-29 09:00:11| CRI

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia uungaji mkono wa operesheni za umoja huo Bw. Atul Khare, amekamilisha ziara ya siku tatu nchini Somalia Jumapili iliyopita akisisitiza haja ya ufadhili zaidi kuunga mkono vikosi vya usalama vya Somalia. Ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuufadhili Mfuko wa Udhamini unaosimamiwa na shirika hilo, na kuomba raslimali zaidi kutolewa ili kuhimiza juhudi za kuleta utulivu nchini Somalia.

Bw. Khare ametambua kazi muhimu iliyofanywa na Ofisi ya Usaidizi wa UM nchini Somalia (UNSOS) ambayo imesaidia serikali ya Somalia kuimarisha uwezo wa vikosi vyake na sekta mbalimbali za kuhudumia raia, alisema sasa ukosefu wa raslimali katika Mfuko wa Udhamini unaosimamiwa na UNSOS, umeleta vizuizi katika kuongeza idadi ya vikosi vya usalama vinavyofadhiliwa nchini humo.