Burkina Faso imejiandaa kwa matokeo ya kujitoa ECOWAS
2024-01-30 23:32:20| cri

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Diaspora wa Burkina Faso, Karamoko Jean Marie Traore amesema, nchi hiyo itafanya kazi kupunguza matokeo hasi ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Akizungumzia matokeo ya hatua hiyo kupitia kituo cha televisheni ya taifa cha nchi hiyo, RTB, Bw. Karamoko amesema, ushirikiano na nchi nyingine wanachama wa ECOWAS unajumuisha maeneo mbalimbali.

Jumapili iliyopita, Mali, Burkina Faso, na Niger zilitoa taarifa ya pamoja kuhusu kujitoa ECOWAS, jumuiya ya kikanda yenye nchi wanachama 15.