Ushirikiano kati ya China na Zimbabwe waboresha maendeleo ya raslimali watu
2024-01-30 08:31:48| CRI

Maofisa wa serikali ya Zimbabwe wamesema ushirikiano kati ya China na Zimbabwe katika kujenga uwezo wa watu umeimarisha maendeleo ya raslimali watu nchini Zimbabwe.

Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Zimbabwe Bibi Mercy Dinha, amesema athari za ushirikiano huu zimekuwa kubwa, na kuhimiza maendeleo ya maofisa na wataalamu ambao wamechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yao.

Bibi Dinha amesema hayo kwenye hafla ya ushirikiano wa maendeleo ya rasilimali watu kati ya China na Zimbabwe iliyofanyika kwenye Ubalozi wa China mjini Harare. 

Amesema historia ya miongo mingi ya ushiriki wa China katika maendeleo ya raslimali watu nchini Zimbabwe, inaonyesha kwa kina kujitolea kwa China katika kuzipatia nchi zinazoendelea ujuzi, utaalamu na raslimali.