UM: Watu 54 wauawa kwenye mapigano yaliyoibuka Abyei kati ya Sudan na Sudan Kusini
2024-01-30 08:21:16| CRI

Taarifa iliyotolewa jumatatu na Kikosi cha Usalama cha Muda cha Umoja wa Mataifa huko Abyei (UNISFA) inasema raia 52 na walinda amani wawili wameuawa kwenye mapigano kati ya jamii katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei linalogombewa na Sudan na Sudan Kusini.

UNISFA imesema inashirikiana na mamlaka za eneo hilo kuthibitisha idadi ya vifo, majeruhi na wakazi waliokimbia mapigano, na kuweka idadi ya sasa ya vifo na majeruhi kwa raia kuwa 52 na 64 mtawalia.

UNISFA imelaani vikali mashambulizi haya dhidi ya raia na walinda amani, ikisisitiza kuwa vurugu dhidi ya walinzi wa amani zinachukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa. Pia imesema inafanya kila juhudi kurejesha utulivu na kulinda raia, na kutaka uchunguzi ufanyike mara moja ili kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.