China yampongeza Bw. Azali Assoumani kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Comoro
2024-01-30 08:20:38| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China inampongeza Bw. Azali Assoumani kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Comoro kwa muhula mwingine.

Msemaji huyo amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa Rais Assoumani, Comoro itapata mafanikio makubwa zaidi kwenye ujenzi wa taifa na maendeleo ya uchumi na jamii. China siku zote inatilia maanani kukuza uhusiano wa kirafiki na Comoro na inapenda kufanya jitihada pamoja na serikali mpya ya nchi hiyo katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kutoa msukumo mpya katika maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.