Tanzania yajiandaa kufanya mageuzi sekta ya sanaa
2024-01-30 14:54:36| cri

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya nchini Tanzania imesema, wadau 800 wa utamaduni na sanaa nchini humo wanatarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili masuala yanayoathiri sekta hiyo.

Katibu mkuu wa Wizara hiyo Gerson Msigwa, amewaambia wanahabari jana kuwa, mkutano huo unalenga kukutanisha wadau muhimu wa sekta hiyo watakaojadili masuala yao na changamoto, kujenga mtandao, na kubadilishana uzoefu ili kuiendeleza zaidi sekta hiyo.

Aidha, Msigwa amesema, katika mkutano huo watajadili hali ya sekta ya utamaduni na Sanaa nchini humo na kutoa mapendekezo ya maboresho, kujadili changamoto na mikakati ya kuzitatua changamoto hizo, na kutambua na kuwazawadia wadau waliofanya vizuri katika sekta hiyo.