OCHA yahitaji dola bilioni 1.6 kusaidia watu milioni 5.2 nchini Somalia
2024-01-30 08:49:38| Cri


 

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema inahitaji dola bilioni 1.6 za Kimarekani ili kukidhi mahitaji ya watu milioni 5.2 nchini Somalia kwa mwaka huu, kiasi ambacho kimepungua kwa karibu asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Katika ripoti yake ya kila mwezi inayotolewa mjini Mogadishu, OCHA imesema idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu kwa mwaka huu nchini Somalia, imepungua kutoka milioni 8.25 mwaka jana hadi milioni 6.9 kwa mwaka huu.

OCHA imesema mwaka huu mahitaji ya msaada wa kibinadamu yataendelea kuwa makubwa nchini humo kutokana na changamoto za mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na maafa ya hali ya hewa kama vile ukame na mafuriko, migogoro na kukosekana kwa usalama, umaskini, na milipuko ya magonjwa.