Changamoto wanazokumbana nazo wagonjwa wa saratani na njia za kuweza kukabliana nazo
2024-02-02 08:00:10| CRI

Kawaida katika miezi miwili ya mwanzo ya kila mwaka unakuwa wakati wa kutoa elimu juu ya ugonjwa hatari na unaosababisha vifo vingi duniani hasa vifo vya wanawake. Huu si ugonjwa mwingine bali ni saratani. Ugonjwa huu umewafanya watafiti na madaktari kukuna vichwa ili kupata angalau njia ya kutibu kabisakabisa ugonjwa na kuondoa hatari ya kurejea tena kwa mtu aliyewahi kuugua ugonjwa huu, lakini bahati mbaya hadi sasa bado hawajapata jibu. Kwa wale wanaobahatika kupona mara nyinyi inakuwa kwa muda tu ambao wataalamu wanakadiria ni miaka mitano na baada ya hapo hurejea tena.

Tukiwa tupo katika kipindi cha kutoa hamasa kwa waathirika wa saratani ama watu wanaowauguza wagonjwa, na sisi tunaona itakuwa heri kama tukitoa nasaha zetu kupitia kipindi hiki. Watu wnaoogua ugonjwa huu katika kipindi chote cha tiba huwa wanapitia mchakato mrefu sana wenye changamoto nyingi za kijamii, kibaolojia na kiuchumi. Kwa maana hiyo mbali na mambo mengine leo katika ukumbi wa wanawake tutaangalia changamoto hizi wanazokumbana nazo wagonjwa na kujua njia gani za kuweza kukabliana nazo. Pia tutasikia ushuhuda wa watu mbalimbali ambao wameugua ugonjwa huu.