Rais Xi aipongeza Nauru kwa kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru
2024-01-31 14:19:24| cri

Rais Xi Jinping wa China leo Jumatano ametoa salamu za pongezi kwa mwenzake wa Nauru David Adeang kufuatia nchi hiyo kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru.

Kwenye salamu zake, rais Xi amesema China na Nauru tayari zimerejesha uhusiano wa kibalozi, na zinafungua ukurasa mpya wa uhusiano wao. Amemsifu rais Adeang kwa kufanya uamuzi wenye busara za kisiasa wa kutambua sera ya kuwepo kwa China moja.

Rais Xi ameeleza kutilia maanani kuendeleza uhusiano kati ya China na Nauru na anapenda kufanya juhudi na rais Adeang, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano wa kivitendo na mawasiliano ya kitamaduni ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.