Madaktari wa Zanzibar wafanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza wa kutumia darubini kwa msaada wa madaktari wa China
2024-01-31 14:36:12| cri

Kundi la 33 la madaktari wa China limefanikiwa kuwafundisha madaktari wa Tanzania Zanzibar kufanya upasuaji wa kwanza kwa kutumia darubini.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameishukuru timu ya madaktari wa China, akisema sio kwamba wamefanya upasuaji kadhaa, lakini pia wamesaidia kupanua wigo wa uelewa wa kitaalamu kwa madaktari wa huko.

Kiongozi wa madaktari wa China visiwani Zanzibar, Jiang Guoqing amesema, tangu mwezi Juni mwaka 2022, timu ya madaktari wa China Visiwani humo iliamua kuboresha mafunzo kwa madaktari wa upasuaji wa huko katika ufundi wa upasuaji wa kutumia darubini. Amesema baada ya mafunzo, madaktari wa Zanzibar walifanya upasuaji wa kwanza na kuukamilisha kwa kujitegemea.

Mmoja wa madaktari wa Zanzibar aliyeshiriki kwenye upasuaji huo, Dr. Rashid Masoud Said ameishukuru timu ya madaktari wa China kwa mwongozo wao.