Rais Xi Jinping ampongeza Bw. Azali Assoumani kuchaguliwa kuwa Rais wa Comoro kwa muhula mwingine
2024-01-31 08:24:08| CRI

Rais Xi Jinping wa China Januari 28 alizungumza kwa njia ya simu na Bw. Azali Assoumani, akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Comoro kwa muhula mwingine.

Rais Xi amesema China na Comoro ni marafiki wakubwa, wenzi na ndugu wazuri wanaoaminiana kwa udhati. Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepiga hatua kwa kasi na ushirikiano wa kiutendaji kati ya pande hizo mbili umezaa matunda kwenye nyanja mbalimbali. China na Comoro zimekuwa zikiungana mkono kithabiti kwenye masuala yanayohusiana na maslahi ya upande mwingine na yale yanayofuatiliwa na upande mwingine. Rais Xi amesema anatilia maanani uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na anapenda kushirikiana na Rais Assoumani katika kusukuma mbele uhusiano wa nchi zao ufikie ngazi ya juu zaidi, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.