China yashirikiana na pande mbalimbali kutoa mchango kutuliza mvutano wa Bahari ya Sham
2024-01-31 08:23:07| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema China haitaki mvutano uendelee katika Bahari ya Sham, inatoa wito wa kusitisha vitendo vya kusumbua au kushambulia meli za kiraia, lakini pia inataka mamlaka ya nchi za Bahari ya Sham ikiwemo Yemen iheshimiwe kihalisi, na inashirikiana na pande mbalimbali kwenye juhudi za kutuliza mvutano wa eneo hilo.

Msemaji huyu pia amezitaka pande hasimu kwenye ukanda wa Gaza zitekeleze kivitendo maazimio husika ya Umoja wa Mataifa, na kusitisha vita mara moja, na kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya uratibu kufanikisha lengo hili.