Kitovu cha Pan-Afrika chazinduliwa nchini Kenya ili kuboresha huduma za afya ya msingi
2024-02-01 08:37:07| CRI

Wizara ya Afya ya Kenya kwa ushirikiano na asasi ya mambo ya afya VillageReach, imezindua Kituo cha Kikanda cha Afrika huko Nairobi, ili kubadilisha utoaji wa huduma za afya ya msingi.

Mkuu wa Kurugenzi ya Uhamasishaji Afya na Elimu katika Wizara ya Afya Bibi Gladys Mugambi, amesema kituo hicho kinalenga kutumia zana za kidijitali, ushirikishwaji wa jamii, kutoa elimu rika na ushirikiano katika jitihada za kuhakikisha kuwa huduma za kinga na uhamasishaji zinapatikana kwenye maeneo magumu kufikika.

Amesema kituo hicho kitahimiza uvumbuzi, utafiti na ushirikiano unaohitajika ili kufikia afya kwa wote katika bara zima.

Bibi Mugambi amebainisha kuwa Kenya imepitisha mfumo wa sheria na sera, na kutumia data na teknolojia zinazoibuka katika jitihada za kuleta mapinduzi kwenye huduma za afya katika pande mbalimbali za nchi.