UM, Ubalozi wa China nchini Kenya waandaa tamasha la Sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China
2024-02-01 08:24:50| CRI

Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa China nchini Kenya na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) wameandaa tamasha la kukaribisha Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina mjini Nairobi.

Kwenye tamasha hilo liliohudhuriwa na maofisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na wasomi, katibu mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Bibi Zainab Hawa Bangura, amesema kwa mara ya kwanza Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina imetambuliwa na kuingizwa kwenye kalenda ya sikukuu ya Umoja wa Mataifa. Ofisa huyo ameeleza matumaini yake kuwa sikukuu hiyo italeta amani, furaha, afya njema na ustawi kwa binadamu.