Ethiopia yazuia mashambulizi 4,550 ya mtandaoni ndani ya miezi sita
2024-02-01 08:25:43| CRI

Ethiopia imezuia zaidi ya mashambulizi 4,550 ya mtandaoni ndani ya miezi sita ya kwanza katika mwaka wa fedha wa 2023/24, ulioanzia Julai.

Katibu mkuu wa Mamlaka ya Usalama wa Mtandao nchini Ethiopia (INSA), Bw. Solomon Soka amesema mamlaka yake imefanikiwa kuzuia zaidi ya asilimia 98 ya mashambulizi yote 4,623 ya mtandaoni dhidi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ofisa huyu mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya Ethiopia yameongezaka kwa asilimia 115 kuliko mwaka uliopita wa fedha, hali inayochangiwa na matumizi mapana ya teknolojia ya dijitali duniani, kuongezeka kwa faida wanazopata washambuliaji, na maendeleo ya kasi ya miundombinu ya dijitali nchini Ethiopia.