AfDB yasema uwekezaji wa China kwenye miundombinu wachochea ukuaji barani Afrika
2024-02-02 08:22:04| CRI

Katibu Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Vincent Nmehielle amesema uwekezaji mkubwa wa China kwenye miundombinu barani Afrika unachochea ukuaji wa uchumi wa bara hilo.

Bw. Nmehielle amewaambia wanahabari mjini Nairobi, kwamba China imefadhili miradi ya miundombinu kupitia mikataba ya pande mbili na nchi za Afrika, na pia kupitia taasisi za fedha za maendeleo za pande nyingi, na kutarajia kuwa miradi hiyo inaweza kufungua uchumi kwa namna ya kuziwezesha nchi kufanya kazi, ikiwa ni pamoja na barabara au madaraja ambayo hurahisisha usafirishaji wa bidhaa.

China na AfDB zilianzisha kwa pamoja mfuko wa kuhimiza maendeleo ya Afrika, ili kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika, mfuko ambao umekuwa ni kichocheo kwa ukuaji.