Kenya yazindua mfuko kuunga mkono operesheni za kulinda amani
2024-02-02 08:23:54| CRI

Kenya imezindua mfuko wa kitaifa wa kuunga mkono operesheni za kulinda amani wenye lengo la kuhakikisha vikosi vilivyotumwa kwenye maeneo yenye migogoro ya kikanda au duniani, vinapata raslimali na vifaa vinavyohitajika.

Waziri wa Ulinzi wa Kenya Bw. Aden Duale amesema mfuko huo uliopitishwa na Baraza la Mawaziri mwezi Oktoba mwaka 2023, utaisaidia Kenya kutekeleza ahadi yake ya kulinda amani na utulivu katika nchi za nje.

Bw. Duale amesema katika miaka ya hivi karibuni, mchango wa Kenya kwa operesheni za kulinda amani umekumbwa na ukosefu wa raslimali, akiainisha kuwa uhamasishaji wa ndani wa raslimali utakuwa muhimu katika kutoa vifaa vinavyohitajika kwa vikosi vinavyotumwa kwenye maeneo yenye migogoro nje ya nchi.