Kikao cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China chafanyika
2024-02-02 16:46:28| cri

Kikao cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimefanyika mwisho wa mwezi Januari chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, Xi Jinping.

Mkutano huo umesikiliza ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC baada ya kusikiliza na kujadili ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la Taifa, Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, Mahakama Kuu ya China, na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu ya China, na ripoti ya kazi ya Sekretariet ya Kamati Kuu ya CPC.

Washiriki wa mkutano huo pia walijadili muhtasari wa ripoti ya Utekelezaji wa Mawazo ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalumu wa China kwa Zama Mpya.

Mkutano huo ulithibitisha kikamilifu kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, Mahakama Kuu ya China, pamoja na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC tangu mkutano wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kukubaliana na mipango yao ya kazi ya mwaka 2024.