China kutoa mafunzo kwa maofisa wa Sudan Kusini kuhusu ujenzi wa uwezo mwaka 2024
2024-02-02 08:24:27| CRI

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Ma Qiang amesema China itaandaa semina sita za mafunzo ya ujenzi wa uwezo kwa maofisa wa Sudan Kusini mwaka 2024 kuhusu maendeleo ya raslimali watu.

Akiongea kwenye hafla ya kukaribisha Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina na kujumuika tena na washiriki wa Sudan Kusini walioshiriki kwenye programu za mafunzo za serikali ya China za mwaka 2023, iliyofanyika katika Ubalozi wa China mjini Juba, Balozi Ma amesema, mwaka huu serikali ya China itaendelea kuimarisha ushirikiano kwenye maendeleo ya raslimali watu na Sudan Kusini, yakihusisha semina sita za mafunzo kuhusu kilimo, elimu, biashara, uchukuzi na mafuta na nyinginezo.

Mwaka 2023 maofisa wa serikali na wataalamu wa kiufundi zaidi ya 300 kutoka Sudan Kusini walishiriki kwenye programu mbalimbali za mafunzo nchini China.