Milipuko mikubwa imeripotiwa huko Embakasi, Nairobi
2024-02-02 16:37:35| cri

Milipuko iliripotiwa dakika chache baada ya saa sita usiku karibu na Skyline Estate huko Embakasi, Nairobi. Wakaazi wa eneo hilo walishangazwa na milipuko mikubwa iliyosikika katika eneo hilo, hali iliyozua wasiwasi na hofu kubwa.

Taarifa zinaeleza kuwa milipuko hiyo ilitokea baada ya gesi kuvuja na kusababisha moto mkubwa kuteketeza eneo hilo kwa haraka. Wakazi wachache walifanikiwa kunasa tukio hilo la kutisha kwenye kamera, huku picha zikionesha miale mirefu ya moto na moshi mnene ukipanda angani, na kutoa kivuli cha kutisha kwenye nyumba za ghorofa zilizo karibu.

Timu za dharura, ikiwa ni pamoja na wazima moto na watumishi wa afya, wamepelekwa haraka kwenye eneo la tukio kudhibiti moto na kutoa msaada kwa walioathiriwa.