Ushoroba salama ulioanzishwa na UM mashariki mwa DRC wawaokoa raia dhidi ya mapigano makali
2024-02-02 08:52:58| CRI

Msemaji mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema ushoroba salama uliowekwa na walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umesaidia kuokoa raia zaidi ya elfu moja kutokana na mapigano makali yanayoendelea nchini humo.

Amesema walinda amani hao kutoka tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa (MONUSCO) walitumwa katika jimbo la Kivu Kaskazini na kujenga kituo cha muda huko Mweso kwa ajili ya ukanda wa kibinadamu, wakati wa mapambano kati ya kundi la waasi la M23 na jeshi la DRC. Ameongeza kuwa MONUSCO pia inaendelea kulinda na kutoa msaada wa kimatibabu kwa wakimbizi walioko Kitchanga, kilomita 15 mbali na Mweso.