Rais Xi atoa salamu za sikukuu ya mwaka mpya wa jadi kwa Wachina wote
2024-02-02 21:51:46| cri

Rais Xi Jinping ametoa salamu za sikukuu ya mwaka mpya wa jadi kwa watu wote wa China, wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Manispaa ya Tianjin kaskazini mwa China kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa.

Rais Xi, ambaye pia Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati Kuu ya Kijeshi, amewatakia Wachina wa makabila yote, ndugu wa Hong Kong, Macao na Taiwan, na Wachina wa ng'ambo afya njema na furaha katika Mwaka wa dragon, na ustawi wa nchi.