UM waahidi kutoa mafunzo ya kiufundi kwa vikosi vya usalama vya Somalia
2024-02-05 10:58:11| cri

Tume ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) imeahidi kutoa mafunzo ya kiufundi kwa vikosi vya usalama vya nchini humo wakati wa kipindi cha mpito.

Tume hiyo inayotoa msaada wa ugavi kwa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jumamosi mjini Mogadishu, kuwa mafunzo hayo yatahakikisha operesheni endelevu na utunzaji wa vifaa vya vikosi vya usalama.

Ofisa msimamizi wa UNSOS Qurat-Ul-Ain Sadozai amesisitiza makabidhiano salama ya kambi saba za kijeshi wiki iliyopita, na kupongeza uhusiano kati ya ATMIS, serikali ya Somalia na Tume yake, huku akiahidi kuendeleza uratibu na uungaji mkono wa zoezi hilo.