Rais mpya wa Namibia aapishwa
2024-02-05 10:57:30| cri

Rais mpya wa Namibia, Nangolo Mbumba jana ameapishwa kuwa rais wa nne wa taifa hilo baada ya rais wa nchi hiyo, Hage Geingob kufariki mapema siku hiyo.

Kiongozi huyo aliyewahi kuhudumu kama makamu wa rais chini ya Serikali ya Rais Geingob ameapishwa katika Ikulu ya nchi hiyo. Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Rais Mbumba ametoa pongezi kwa mtangulizi wake akimtaja kuwa mbunifu mkuu wa katiba na usanifu wa utawala wa Namibia.

Mbumba ameapishwa kuwa Rais wa Namibia na Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Namibia na atakuwa Rais hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika baadaye mwaka huu.