Chuo Kikuu cha Rwanda chafanya hafla ya kusherehekea Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China
2024-02-05 09:39:06| CRI

Hafla ya kiutamaduni ya kusherehekea Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China wa dragon inayokaribia kufika ilifanyika mjini Kigali, Rwanda.

Hafla hiyo ilifanyika katika Taasisi ya Confucius iliyoko katika Chuo Kikuu cha Rwanda, na wengi walioshiriki ni wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kichina kwenye taasisi hiyo. Shughuli zilizofanyika kwenye hafla hiyo ni pamoja na mhadhara unaoeleza Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, sanaa ya ukataji wa karatasi, na kuandika maneno ya Kichina yanayomaanisha baraka na furaha.

Mkurugenzi wa China kwenye Taasisi ya Confucius Zeng Guangyu alisema hafla hiyo inalenga kuwafundisha wanafunzi utamaduni wa China na kuwafanya wahisi mazingira ya mwaka mpya wa jadi wa China.