Xi atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha rais Geingob wa Namibia
2024-02-06 10:49:32| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kwa Rais mpya wa Namibia aliyeapishwa Nangolo Mbumba kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Namibia Hage Geingob.

Kwa niaba ya serikali na watu wa China, na yeye mwenyewe, rais Xi alitoa salamu za rambirambi na kutoa pole kwa serikali ya Namibia na watu wake, pamoja na familia ya Geingob.

Katika salamu zake, rais Xi alisema kwamba kiongozi bora wa Namibia Rais Geingob amehimiza maendeleo makubwa ya ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya China na Namibia na kutoa mchango mkubwa katika kukuza urafiki wa China na Namibia na Afrika. Kifo chake ni hasara kubwa kwa watu wa Namibia, na pia Wachina wamempoteza rafiki mzuri.

Ameongeza kuwa China inathamini urafiki wa jadi kati ya China na Namibia na iko tayari kushirikiana na Namibia ili kusukuma mbele maendeleo endelevu ya ushirikiano wa kimkakati wa nchi hizo mbili.