Biashara ya kaboni kuinufaisha zaidi Tanzania
2024-02-06 10:10:20| cri

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) nchini Tanzania, Selemani Jafo amesema, serikali ya nchi hiyo inatarajia kupata wastani wa shilingi trilioni 2.4 kutokana na biashara ya kaboni ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa.

Akizungumza bungeni jana mjini Dodoma, Waziri Jafo amesema hadi kufikia Desemba 31, 2023 serikali imepokea jumla ya maombi 35 ya miradi mbalimbali ya biashara hiyo pindi mchakato wa usajili utakapokamilika na kuanza kutekelezwa kwa miradi hii.

Ameongeza kuwa, Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamasisha kupanda miti kwa wingi ili kunufaika na biashara hiyo na kuhifadhi mazingira.