Tunisia yazuia majaribio 99 ya uhamiaji haramu ndani ya wiki moja
2024-02-06 10:09:40| cri

Tunisia imezuia majaribio 99 ya wahamiaji haramu kuvuka Bahari ya Mediterranean kwenda Italia katika wiki moja iliyopita.

Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha Tunisia kimesema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook kwamba, askari wa ulinzi wa pwani wa nchi hiyo wamezuia majaribio hayo katika pwani za nchi hiyo na kuokoa wahamiaji haramu 2,469 kati ya Januari 28 na Februari 3 mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema, wahamiaji haramu waliookolewa ni pamoja na raia 2,064 wa nchi tofauti za Afrika na raia 405 wa Tunisia.