Moto mkubwa wa msituni katikati mwa Chile wasababisha vifo vya watu 122
2024-02-06 10:40:07| CRI

Serikali ya Chile Jumatatu ilisema moto mkubwa wa msituni huko Valparaiso, katikati mwa nchi hiyo umesababisha vifo vya watu wasiopungua 122.

Kutokana na idara ya uchunguzi wa kisheria ya nchi hiyo, wahanga 32 tu wametambuliwa, na timu za wataalamu zimefanya uchunguzi wa miili 40.

Moto mkubwa ulitokea Ijumaa kwenye maeneo tofauti umeteketeza hekta zaidi ya elfu 11 huko Valparaiso, na kati ya nyumba elfu tatu na elfu sita zimeharibiwa kwa viwango tofauti. Chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.

Serikali ya huko imetangaza kuingia katika hali ya tahadhari, na kusambaza vikosi vya kijeshi ili kuudhibiti na kusafirisha rasilimali za ziada kwenye eneo hilo.