Mkutano wa Uchimbaji Madini wa Indaba wafunguliwa Cape Town huku kukiwa na wito wa ushirikiano ili kukabiliana na changamoto
2024-02-06 10:46:50| CRI

Mkutano wa Uchimbaji Madini wa Indaba 2024 ulianza Jumatatu mjini Cape Town, ambapo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Mkutano huo wa 30 wa Uwekezaji katika Madini wa Afrika, uliofanyika chini ya kaulimbiu "Kukumbatia nguvu ya usumbufu chanya: mustakabali mpya wa ujasiri wa uchimbaji madini wa Afrika," unatarajiwa kuendelea hadi Alhamisi na kuvutia wajumbe 10,000, wakiwemo kutoka mamia ya sekta nzito. Neno "Indaba" linatokana na lugha ya Kizulu, likimaanisha mkutano wa kujadili mada nzito.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi Jumatatu, iliyohudhuriwa pia na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sama Lukonde pamoja na mawaziri na naibu mawaziri kutoka katika bara la Afrika, Ramaphosa alisema kuwa uchimbaji madini umekuwa nguzo ya uchumi wa Afrika Kusini kwa karibu miaka 150.

Kwa mujibu wake, sekta ya madini inachangia asilimia 7.5 katika pato la taifa la Afrika Kusini (GDP) na inachangia asilimia 60 ya mauzo ya nje ya nchi kwa thamani.