Watu 26 wauawa katika mapigano mapya nchini Sudan Kusini
2024-02-07 10:56:35| cri

Watu 26 wameuawa katika mapigano mapya ya kikabila magharibi mwa Sudan Kusini, huku rais na makamu wa rais wa nchi hiyo wakitoa wito wa kumaliza mapigano ya kikabila nchini humo.

Maofisa wa huko wamesema, zaidi ya watu 150 wameuawa tangu wiki iliyopita katika mapigano tofauti yaliyohusisha vijana kutoka mkoa wa Warrap dhidi ya wapinzani wao kutoka mikoa jirani ya Lakes na Western Bar El Ghazal, na mkoa wa Abyei unaoendeshwa kwa pamoja na Sudan na Sudan Kusini.

Maofisa hao wamesema, mapigano hayo hayaonekani kuwa na uhusiano wa moja kwa moja, bali yote yanahusiana na udhibiti wa ardhi na maliasili.