Waziri Mkuu wa Qatar asema Hamas imetoa jibu zuri juu ya makubaliano ya kuwaachia huru mateka
2024-02-07 08:37:14| CRI

Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani amesema kuwa Qatar imepokea jibu zuri kutoka kwa Hamas kuhusu pendekezo la makubaliano ya kuwaachia huru mateka ili kusitisha mapigano huko Gaza .

Aliyasema hayo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken aliyepo ziarani nchini humo.

Kuhusu majibu ya Hamas, waziri mkuu wa Qatar hakutoa maelezo zaidi. Blinken pia amethibitisha kuwa maafisa wamepokea majibu ya Hamas na atayajadili na viongozi wa Israel wakati wa ziara yake nchini Israel. Blinken ameongeza kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanywa, na anaamini kuwa makubaliano yanawezekana kufikiwa.