Mamlaka za kupambana na dawa za kulevya Tanzania Zanzibar zimesema zimekamata kilo 125 za aina tofauti za dawa za kulevya, ikiwemo heroin na bangi, na kuwakamata watu 19 wanaoshukiwa kuhusika na dawa hizo.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa ya Tanzania Zanzibar imesema, dawa hizo za kulevya zimekamatwa katika mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja.
Taarifa hiyo pia imesema mamlaka hiyo imekamata magari saba, boti mbili, na simu mbili zinazotumia satelaiti, kompyuta ya mkononi, na kifaa cha GPS ambavyo vinatumika kusafirisha dawa hizo nje ya nchi.