Rais Xi Jinping atoa pongezi kwa kukamilika, uendeshaji wa Kituo cha Qinling katika eneo la Antaktika
2024-02-07 15:53:44| cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Qinling na kuanza kwake kufanya kazi huko Antaktika.

Kituo cha Qinling ni kituo cha tano cha utafiti nchini Antaktika, kilianza kufanya kazi siku ya Jumatano.

Rais Xi ametoa salamu zake za dhati na salamu za Mwaka Mpya wa China kwa watu wanaofanya kazi kwenye utafiti wa ncha ya dunia.

Pia amesema mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 40 ya safari ya China kwenye ncha za dunia, na kuwa utafiti wa eneo la ncha ya dunia umepata matokeo mazuri, kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Qinling kutatoa uhakikisho mkubwa kwa wanasayansi nchini China na duniani kote kuendelea na uchunguzi.

Rais Xi pia ametoa mwito wa uelewa zaidi, ulinzi na matumizi ya maeneo ya ncha na kutoa mchango mpya na mkubwa zaidi kwa manufaa ya binadamu na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.