Karibu asilimia 90 ya watu waliohojiwa duniani wasema mpasuko ndani ya Marekani unaweza kuwa jambo la kawaida
2024-02-08 10:21:16| CRI

Wahamiaji wanaendelea kutekeseka huku mvutano wa kisiasa ukizidi kuwa mkali nchini Marekani. Hivi sasa kuna mzozo mkubwa kati ya serikali ya jimbo la Texas na serikali kuu kuhusu suala la uhamiaji, huku watu wengine wakiutaja kama "talaka ya taifa".

Kwa mujibu wa kura ya maoni duniani iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Televisheni la China CGTN, asilimia 86.5 ya watu waliohojiwa wanaamini kwamba makabiliano kati ya pande hizo mbili kuhusu uhamiaji kwa mara nyingine tena yanaonesha ukweli kwamba vyama viwili nchini Marekani vinazidisha kushindana kwao na siasa zinazidi kukosa mpangilio.

Kwa muda mrefu uhamiaji limekuwa suala la mzozo kati ya vyama vya Republican na Democratic nchini Marekani. Ili kukwepa majukumu yao ya kisiasa, vyama hivyo viwili vimefikia hatua ya “kupelekeana wahamiaji”.

Katika utafiti huo, asilimia 70.2 ya wahojiwa duniani walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu ghasia na tabia ya kikatili ya serikali ya Marekani katika kushughulikia wahamiaji, na kuamini kuwa maafisa wa sheria wa Marekani wamekiuka kwa kiasi kikubwa haki za msingi za binadamu za wahamiaji.