Timu ya maafikiano ya Umoja wa Afrika yaenda Somalia kuhakikisha mpito wa amani
2024-02-08 23:06:07| cri

Wajumbe wa Mfumo wa Uwajibikaji na Maafikiano wa Umoja wa Afrika (AUCF) wamefanya ziara nchini Somalia kwa lengo la kuboresha juhudi za ulinzi wa raia kabla ya Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kuondoa askari wake nchini humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Tume hiyo imesema ujumbe wa AUCF unaoongozwa na Adebayo Kareem jumanne ulifanya mazungumzo na kamanda wa ATMIS Sam Okiding, uongozi wa kijeshi wa Tume hiyo, na makamanda wa vikosi mbalimbali, yaliyolenga kanuni zilizorekebishwa hivi karibuni na Umoja wa Afrika kuhusu kuondoa askari wake nchini Somalia.

ATMIS imesema, kama sehemu ya ziara yao ya wiki moja nchini Somalia, ujumbe huo utafanya mazungumzo na wadau mbalimbali, wakiwemo maofisa wa serikali, ATMIS, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia ili kuimarisha zaidi ulinzi wa raia wakati wa mchakato wa mpito.