Xi atoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa watu wasio wanachama wa CPC
2024-02-08 09:53:44| CRI

Rais wa China na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti (CPC), Xi Jinping ametoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wasio wa CPC na Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC), watu wasio na vyama, na watu wenye nia moja walio mstari wa mbele kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China

Katika salamu hizo alizozitoa wakati aliposhiriki katika hafla ya kila mwaka na wanachama wasio wa CPC kwenye Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Umma hapa Beijing, rais Xi alisema mwaka 2023 ulikuwa mwaka wa kushangaza. Kwa mwaka mzima, Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ilikiongoza Chama kizima na watu wa China kutekeleza kikamilifu kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na kufanyia kazi kanuni za jumla za kutafuta maendeleo huku kikihakikisha utulivu.

Aidha amebainisha kuwa China ilihimili shinikizo la nje na kushinda matatizo ya ndani, ilifanya juhudi za kila namna ili kuinua uchumi na maendeleo, na kufanikiwa kufikia malengo makuu yaliyowekwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.