Makamu wa Rais wa Tanzania azitaka serikali za Afrika kushughulikia changamoto za ajira
2024-02-08 09:17:41| CRI

Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango amezitaka serikali za Afrika kukabiliana na changamoto zinazohusiana na utoaji wa nafasi za ajira, akisema zinahitajika mbinu jumuishi, mageuzi na shirikishi

Akifungua Mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii wa Afrika Jumatano jijini Dar es Salaam, Mpango alibainisha kuwa utoaji wa ajira na mikakati inayohimiza ukuaji na maendeleo shirikishi vimekuwa vipaumbele muhimu vya serikali zote za Afrika.

Aliongeza kuwa mikutano ya Kilele ya Washirika wa Kijamii ya Afrika imetoa maarifa na miongozo ya kukuza fursa za ajira kote Afrika.

Mpango alisema changamoto za ajira barani Afrika zimechangiwa zaidi na msukosuko wa hali ya hewa duniani, athari mbaya za migogoro inayoendelea katika bara la Afrika, athari za mivutano ya kijiografia katika maeneo kadhaa ya dunia, pamoja na athari mbaya za janga la UVIKO-19.