Tanzania yaanza majaribio ya mfumo mpya wa ufundishaji
2024-02-09 23:07:29| cri

Serikali ya Tanzania imeanza majaribio ya mfumo wa ufundishaji mubashara ambapo mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wa nchi nzima kwa wakati mmoja.

Mfumo huo ambao kwa sasa unafanyiwa majaribio katika baadhi ya shule za mikoa miwili ya Pwani na Dodoma nchini humo, unamuwezesha mwalimu kutoka kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa mikoa tofauti.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma wamesema mfumo huo utawasaidia kupata uelewa kwa wepesi na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.