Kenya yarejea ahadi yake ya kuunga mkono juhudi za amani na utulivu wa kikanda
2024-02-09 10:27:28| Cri


 

Waziri wa Ulinzi wa Kenya Aden Duale amerejea tena ahadi ya Kenya ya kuunga mkono juhudi za amani na utulivu wa kikanda.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa jijini Washington, Marekani, Waziri Duale amesisitiza nafasi ya Kenya kama nchi muhimu ya kanda ya Afrika Mashariki, na kusema Kenya inashikilia uwiano kati ya kukabiliana na changamoto za ndani na kuchangia kidhahiri katika juhudi za ulinzi wa amani katika kanda hiyo.

Ametolea msisitizo katika changamoto ya siasa za kijiografia, hususan athari zinazotokana na ukosefu wa usalama katika nchi jirani ya Somalia.