Usafiri wa Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina waonesha uhai wa China
2024-02-09 10:22:18| Cri

Wizara ya Uchukuzi ya China hivi karibuni inakadiria kuwa idadi ya watu watakaosafiri wakati wa Chunyun itafikia bilioni 9, kiwango ambacho kitakuwa rekodi mpya katika historia.

Chunyun, maana yake ni kilele cha usafiri wa abiria wakati wa Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina. Kipindi cha Chunyun cha mwaka huu kitaanzia tarehe 26 Januari hadi tarehe 5 Machi, na kwa jumla ni siku 40. Kulingana na utabiri, kati ya watu bilioni 9 watakaosafiri wakati wa Chunyun, abiria bilioni 1.8 watatumia vyombo vya kiumma ikiwemo reli, mabasi, ndege na meli, na wengine takriban bilioni 7.2 watatumia magari yao ya kibinafsi.

Idadi kubwa ya watu wakati wa Chunyun inaonyesha uhai wa uchumi wa China. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara kuu ya Takwimu ya China zinaonyesha kuwa, mwaka 2023, Pato la Taifa la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na mwaka 2022, na kushika nafasi ya mbele kati ya nchi kubwa ya kiuchumi duniani, ambapo mchango wake kwa ukuaji wa uchumi wa dunia unatarajiwa kuzidi asilimia 30, na kuwa injini kubwa zaidi ya kiuchumi duniani. Chunyun ni safari ya Wachina kurudi nyumbani, na pia ni dirisha la kutazama uchumi wa China. Ongezeko la abiria linaonyesha uahi mkubwa wa uchumi wa China.

Idadi kubwa ya watu wakati wa Chunyun inaonyesha uhai wa jamii ya China. Usafiri wa makundi makubwa ya wanafunzi, wafanyakazi na watalii wakati wa Chunyun ni dalili ya uhai mkubwa wa jamii ya China. Chunyun ni mwujiza kutokana na sera ya mageuzi na kufungua mlango. Katika zaidi ya miaka 40 iliyopita, China imepata maendeleo makubwa sana. Kufuatia uboreshaji wa miundombinu, haswa ukamilifu wa mitandao ya barabara, reli na anga, Chunyun imebadilika kutoka "polepole" hadi "kasi kubwa", kutoka "ugumu" hadi "urahisi",  kutoka watu kukaa nyumbani tu, hadi watu kusafiri mara kwa mara. Chunyun imekuwa dirisha la kushuhudia uhai mkubwa wa jamii ya China.

Idadi kubwa ya watu wakati wa Chunyun inaonyesha uhai wa utamaduni wa China. Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina ni sikukuu muhimu zaidi ya jadi ya taifa la China. Wachina wamesherehekea tamasha hilo kwa zaidi ya miaka 4,000. Ingawa sasa Wachina wamezoea kufanya kazi na kuishi nje ya sehemu ya kuzaliwa kwa muda mrefu, lakini hawaachi desturi ya kurudi nyumbani wakati wa tamasha hilo, hii ni furaha kubwa kwa familia nzima. Pia kuna mabadiliko, licha ya kutembelea wanafamilia na marafiki, sasa Wachina wanapenda kutalii wakati wa tamasha hilo. Huu ni uvumbuzi na maendeleo ya utamaduni wa Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina.