Viongozi 34 wa Afrika na wakuu wa mashirika ya kimataifa kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Afrika
2024-02-09 08:45:41| cri

Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema, takriban viongozi 34 wa Afrika na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika.

Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika, mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 17 na 18 mwezi huu utakuwa na ajenda kadhaa, ambazo ni pamoja na amani na usalama wa bara la Afrika, biashara na mafungamano, elimu na ujuzi, kilimo na mabadiliko ya hali ya hewa, utawala wa nchi na haki za binadamu, pamoja na kuwajengea uwezo vijana na watu wa jinsia zote.