Rais wa China awatakia Wachina wote heri ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina
2024-02-09 09:57:16| Cri


 

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Baraza la Serikali la China zimefanya mkutano wa kubadilishana salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina.

Kwenye mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China amewatakia heri ya mwaka mpya Wachina wa ngazi zote, watu wa Hong Kong, Macao na Taiwan, na Wachina wengine walioko nchi za nje.