Serikali ya Tanzania yaonya matumizi ya dawa za macho kiholela
2024-02-09 10:28:18| Cri


 

Wizara ya Afya nchini Tanzania imetoa tahadhari kwa wananchi kuacha kutumia dawa kiholela, hususani tiba mbadala baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa macho mekundu, ikiwa ni baada ya baadhi ya watu kupata madhara kwenye macho kutokana na matumizi holela ya dawa hizo.

Akizungumza na wanahabari jana mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Wizara hiyo, Prof. Paschal Ruggajo amesema wamepokea taarifa kutoka vituo vya afya kuna ongezeko la wagonjwa wanaofika wakiwa na vidonda kwenye kioo cha mbele cha jicho walizopata baada ya kutumia tiba zisizo rasmi au ambazo hazijaandikwa na daktari rasmi kutubu macho.

Amesema tayari watu 12,332 waliofika katika vituo mbalimbali vya afya nchini humo wamethibitika kupata ugonjwa huo huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuwa na watu 6,412 wanaougua ugonjwa huo.