Tamasha la Spring lavutia watazamaji wa China na Watanzania
2024-02-09 08:47:39| cri

Onesho la wasanii 37 kutoka mkoani Zhejiang nchini China lililofanyika Jumatano usiku jijini Dar es Salam, Tanzania, lilikonga nyoyo za Watanzania na Wachina.

Wasanii wa Tanzania pia walijiunga na wanakikundi cha Sanaa cha Zhejiang kusherehekea Mwaka Mpya wa jadi wa China, katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichojengwa na China.

Maonesho ya wasanii wa China yalikuwa na mchanganyiko wa muziki wa kitamaduni wa Kichina, densi, mazingaombwe, na mengineyo, wakisherehekea urafiki mkubwa kati ya China na Tanzania.

Wasanii wa Tanzania waliwakilishwa na Kundi la Sonda ya Dihlu AcapellaAcapella na Kituo cha Sanaa cha Nimujo. Maonesho yao yalijumuisha ngoma za kisasa na nyimbo na sarakasi zinazoakisi matukio mbalimbali ya jamii ya Kitanzania.

Mwanzilishi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Sanaa cha Nimujo kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, Richard Muro, alisema Mwaka mpya wa jadi wa China umewaonesha ni jinsi gani Wachina wanavyothamini utamaduni wao.